Tazama Mahubiri
Kutimiza agizo kuu kwa kuhubiri Habari Njema, kutoa msaada wa kiroho na kimwili, ili kuunda jamii yenye hofu ya Mungu na inayoishi kwa kufuata sheria na mamlaka.
Kuleta mabadiliko ya maisha kwa kuhubiri Neno la Mungu na kuwasaidia watu kujiandaa kwa ajili ya maisha ya milele.
Ebenezer International Church (E.I.C) ni kanisa la Kipentekoste linaloongozwa na Roho Mtakatifu na limesajiliwa rasmi chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania kwa namba ya usajili S.A.23229. Makao makuu ya kanisa yapo Wilaya ya Kasulu, Mkoa wa Kigoma, na lina matawi mbalimbali ndani ya nchi chini ya uongozi wa Askofu Mkuu Genoveva Charles Ntumo.
Kanisa lilianza mwaka 2011 kama huduma ya maombi na maombezi, na baadaye kuwa kanisa kamili tarehe 12 Julai 2020. Imani kuu ya kanisa ni juu ya Mungu mmoja katika Utatu Mtakatifu – Baba, Mwana na Roho Mtakatifu (Waefeso 4:6).
Tunajitoa kwa moyo katika kuhubiri Habari Njema ya wokovu, kubadilisha maisha ya watu kiroho, na kuwahudumia jamii kijamii na kimwili kupitia idara mbalimbali na mipango ya huduma.
Ili kutekeleza kwa ufanisi dhamira ya kuhubiri Injili na kuhudumia jamii kwa upana, Ebenezer International Church imeunda idara mbalimbali zinazoratibu shughuli za kiroho, kijamii na kiutawala. Kila idara ina jukumu mahsusi la kusaidia katika kuimarisha huduma ya kanisa na jamii kwa ujumla.
Idara hii inahakikisha huduma zote za kiroho, kiutawala, na kijamii zinapangwa, kuratibiwa, na kutekelezwa kwa ufanisi kwa lengo la kufanikisha maono
Idara hii inahakikisha kila shughuli inafanyika kwa mpangilio, uwazi, na kwa kufuata kanuni na maadili ya kanisa
Idara hii inasimamia rasilimali za kifedha, uhasibu, na shughuli zote za utawala ili kuhakikisha kanisa linafanya kazi kwa uwazi, usahihi na ufanisi.
Idara hii inahakikisha mipango yote ya maendeleo ya kanisa inatekelezwa kwa mpangilio mzuri,
Idara hii ipo chini ya uongozi wa Tedy Filimon Jacobo, ambaye anasimamia na kuratibu shughuli zote za wanawake katika kanisa
Kitengo hiki kinahakikisha maombi na maombezi vinaendelezwa kwa utaratibu, viwe na mshikamano, na vinachangia ukuaji wa kiroho wa waumini na maendeleo ya kanisa
Idara hii ina Jukumu la kuhakikisha kwamba injili ya Yesu Kristo inafikishwa kwa watu wote, kanisa linaendelea kusimama imara katika maombi....
Idara hii ina jukumu la kuhakikisha kwamba watoto na vijana wanalelewa katika msingi imara wa kiroho na kijamii
Kutokana na ongezeko la waumini na uhitaji wa nafasi ya kutosha kwa ajili ya ibada, uongozi wa Ebenezer International Church kupitia mkutano mkuu wa mwaka 2024 uliridhia kuanza rasmi mchakato wa ujenzi wa kanisa jipya. Lengo ni kuwa na jengo la kisasa litakalokidhi mahitaji ya huduma za kiroho na kijamii.
Ili kuhakikisha kuna nafasi ya kutosha kwa ujenzi wa jengo jipya na miundombinu ya ziada.
Ramani iliyosanifiwa kitaalamu ili kufanikisha ujenzi unaokidhi viwango vya kisasa.
Maandalizi ya makadirio ya gharama zote za ujenzi ili kurahisisha usimamizi wa rasilimali.
Hii ni pamoja na ruhusa za kisheria na kiutawala zinazohitajika kabla ya kuanza ujenzi.